Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya changamoto Darfur, nilitekeleza jukumu lililonipeleka: SSP Eva

Polisi wanawake katika moja ya hafla kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Abu Shouk. (Picha@Albert González Farran, UNAMID)

Licha ya changamoto Darfur, nilitekeleza jukumu lililonipeleka: SSP Eva

Shughuli za ulinzi wa amani hukutanisha walinda amani na mazingira mapya tofauti na kule walikotoka hata hivyo walinda amani wawe ni askari, maafisa, polisi au watendaji wa kiraia huhakikisha wanajitahidi kutimiza wajibu wao. Miongoni mwao ni Eva Stesheni, Mrakibu msaidizi wa Polisi Tanzania aliyehudumu huko Darfur, Sudan kati ya mwaka 2009 na 2011 kwenye kitengo cha Jinsia na watoto. Eva amemweleza Assumpta MAssoi wa Idhaa hii kuwa changamoto zilikuwa ni nyingi ikiwemo mawasiliano, hali ya hewa lakini alipata matumaini alipoona anabadili kwa njia chanya maisha ya wanawake na watoto. Hapa anaanza na jukumu lake..