Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laongeza muda wa UNMISS na kufanyia marekebisho majukumu yake

Baraza la Usalama

Baraza la Usalama laongeza muda wa UNMISS na kufanyia marekebisho majukumu yake

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limepitisha azimio la kuongeza muda wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, kwa hadi terehe 30 Novemba 2014, na kufanyia marekebisho majukumu ya ujumbe huo.

Katika azimio hilo ambalo pia limeridhia makubaliano ya kusitisha mapigano ya Januari 23 na Mei 9 kati ya serikali ya Sudan Kusini na kundi lililoasi jeshi la kitaifa, SPLM/A (Upinzani), Baraza la Usalama limeamua kuwa majukumu ya UNMISS yatahusisha kuchukua hatua zote kuwalinda raia dhidi ya hatari ya ukatili, bila kujali hatari hiyo inatoka wapi, na hususan ulinzi wa wanawake na watoto.

UNMISS pia itatakiwa kuzuia ukatili dhidi ya raia, wakiwemo raia wa kigeni, kwa kulinda doria, na pia kuwa na mfumo wa kutoa tahadhari mapema ili kuzuia mashambulizi dhidi ya raia, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na majengo na vifaa vyake.