Hali ya usalama CAR yazidi kuzorota, Baraza lapaza sauti
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali kuendelea kuzorota kwa usalama huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ambako mapiganop yaliyoanza upya kati ya majeshi ya serikali na waasi wa kundi la Seleka yanatishia usalama wa raia na mpango wa amani uliotiwa saini mapema mwezi Januari mwaka huu.
Kauli ya baraza hilo inafuatia ripoti iliyowasilishwa na mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Margaret Vogt ambaye alilieleza baraza katika kikao cha faragha kuwa waasi wa Seleka wanadhibiti robo tatu ya nchi na kwamba siku mbili zilizopita waasi katika serikali ya Umoja wa Mataifa walijitoa na kurejea msituni.
Kufuatia taarifa hizo Rais wa Baraza la Usalama Balozi Vitaly Churkin kutoka Urusi akaeleza msimamo wa wajumbe wa baraza hilo.
(SAUTI -1)
Waasi wa Seleka wanadai kuwa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati inashindwa kutekeleza makubaliano ya amani ya Libreville.