Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka kumi tangu mwanamke wa kwanza mwafrika ashinde Nobel, ;Profesa Mathai aenziwa

Ban Ki-moon na Profesa Wangari Maathai (Picha ya UM)

Miaka kumi tangu mwanamke wa kwanza mwafrika ashinde Nobel, ;Profesa Mathai aenziwa

Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa , kumefanyika hafla ya kumuenzi hayati Profesa Wangari Mathai ikiwa ni miaka kumi tangu apokee tuzo ya amani ya Nobel akiwa ni mwanamke wa kwanza mwafrika. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Naibu mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Koki Muli Grinyo amesema Profesa Maathai aligusa maisha ya watu mbali mbali na hata kubadili maisha yao.

Naye Mshauri maalum wa katibu mkuu kwa ajili ya ajenda ya baada ya mwaka 2015 Amina J. Mohammed, akisema kuwa Profesa Maathai alikuwa kielelezo kwa wote waliokutana naye na kwamba sifa zake zitaishi sio tu nchini mwake Kenya lakini mbali zaidi

(Sautiya Amina)

Tunapoangalia ajenda ya baada ya mwaka 2015 ambayo itawezesha maisha yenye hadhi kwa wote, tuchukue hatua kufuata mfano wa Profesa Mathai kwa kujali watu na sayari sawia.”

Hafla hiyo ilijumuisha uzinduzi wa bamba maalum lililonakshiwa taarifa kuhusu Profesa Maathai na upanzi wa mti kando mwa mti aliyepanda Wangari mathai hapa Umoja wa Mataifa.