Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR, DRC na Uganda wajadili urejeshaji wakimbizi wa DRC makwao

UNHCR, DRC na Uganda wajadili urejeshaji wakimbizi wa DRC makwao

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), serikali ya Uganda na wenzao wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wanakutana mjin Kampala kuzungumuzia mpango wa kurejesha nyumbani wakimbizi wa DRC. Taarifa kamili na John Kibego wa radio washirika ya Spice Fm nchini humo

(Ripoti ya John Kibego)

Mkutano huu wa hatua za mwisho za kirejesha nyumbani takribani wakimbizi Elfu Mia Moja na Themanini, (180,000) imekuja mwezi moja baada ya wakimbizi 108 kuzama katika Ziwa Albert wakati wakirejea nyumbani kivyao kutoka kambi ya Kyangwali hapa Uganda.

Naibu Mwakilishi wa UNHCR Uganda Sakura Atsumi, ametaja badhi ya yatakayojadiliwa katika mkutano huu.

(Sauti ya Sakura Atsumi)

“Katika mkutano huu wa siku mbili, tunangazia kwa mfano usafiri wao, nini watajishughulisha nacho pale watakaporejea katika vijiji n vyao?, kuna vyanzo vya maji, mambo kama mbegu, na vifaa”

Musa Ecweru, ni Waziri Mdogo wa kushughulikia majanga na wakimbizi hapa Uganda.

(Sauti ya Musa Ecweru)

Miongoni mwa wajumbe wa DRC, ni Waziri wa mambo ya ndani, usalama na mila Richard Muyaj Magenze Mans

(Richard Muyaj Magenze Mans)