Tutahakikisha amani Guinea Bissau: UM

9 Aprili 2014

Wakati taifa la Guinea Bissau likielekea katika uchaguzi mkuu April 13 mwaka huu, Umoja wa Mataifa umesema uko tayari kusaidia katika kuhakikisha amani na utulivu vinatawala kabla, wakat i na baada ya uchaguzi.

Katika mahojiano maalum na Monica Grayley wa idhaa ya kirusi ya Umoja wa Mataifa, mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa ofisi ya ujumbe wa umoja huo ya kukuza amani nchini Guinea Bissau UNIOGBS, José Manuel Ramos-Horta, kiongozi huyo amesema kipaumbele ni watu wa nchi hiyo.

(SAUTI JOSE)

Hapa Guinea Bissau, tunajarubu kutumia wazo la Umoja wa Mataifa la amani tunawatumikia watu kwa utu lakini tunatakiwa kunyumbulika na kuelewa kwa kuwa tunashulikia hali tete ,watu wenye chuki, wenye hofu na tuhuma. Tunashughulika na wanadamu. Shukrani ni kwa watu wa Guinea Bissau na jumuiya za kikanda kama ECOWAS, Muungano wa Afrika na Ulaya.