Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kizungumkuti Sudan Kusini chazidi, dola Milioni 371 zahitajika kwa usaidizi

Kizungumkuti Sudan Kusini chazidi, dola Milioni 371 zahitajika kwa usaidizi

Wakati hali ya usalama na kibinadamu ikizidi kuzorota huko Sudan Kusini, Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake ya kuhudumia wakimbizi, UNHCR na lile la mpango wa chakula WFP yametoa ombi la usaidizi wa dola Milioni 371 ili kuimarisha huduma zao kwenye eneo hilo.

Ombi hilo linawakilisha pia mahitaji ya wadau wengine wanaoshirikiana na mashiriak hayo katika kusaidia maelfu ya wakimbizi wa Sudan Kusini wanaowasili nchi jirani. UNHCR inatarajia kuwa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu idadi ya wakimbizi hao itafikia 340,000. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

(Sauti ya Adrian)

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mapigano Sudan Kusini yanasababisha raia Elfu Mbili kukimbilia nchi jirani kila siku kusaka hifadhi na huduma muhimu.