Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yazungumzia kuzama kwa wakimbizi wa DRC huko Uganda

UNHCR yazungumzia kuzama kwa wakimbizi wa DRC huko Uganda

Taarifa za kuzama kwa boti iliyokuwa imebeba wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waliokuwepo kwenye kambi ya Kyangwali nchini Uganda imeibua simanzi huku Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, ukieleza kuhuzunika na kushtushwa na taarifa hizo. Boti hiyo ikiwa na mamia ya wakimbizi hao wakiwemo watoto ilizama Jumamosi kwenye Ziwa Albert. John Kibego wa Radio washirika Spice FM alizungumza kwa njia ya simu na Andrew Mbogori, afisa wa UNHCR ambaye amekuwa kwenye harakati za kusaka miili.