Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CSW58 yafikia ukingoni, lengo namba 8 lapigiwa chepuo:

CSW58 yafikia ukingoni, lengo namba 8 lapigiwa chepuo:

Wakati pazia la mkutano wa 58 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani linafungwa hii leo hapa New York, lengo namba nane kuhusu ubia kwa maendeleo limeangaziwa ambapo washiriki wamesema ubia utawezesha kufahamu mbinu mbadala zaidi zinazotumiwa na wengine kuokoa wanawake kutoka lindi la umaskini na tamaduni zinazowakandamizi bila wao kufahamu.

Washiriki hao ni pamoja na Jessica Kamala-Mushala wa shirika la kiraia Shina ambaye ameiambia Idhaa hii mathalani wanajaribu kuelimisha wanawake kuwa si kila tamaduni iliyopo inaweza kumkomboa lakini hatua hiyo itafanikiwa zaidi kupitia ubia na wadau wengine.

(Sauti ya Jessica)

Mahojiano zaidi na Jessica yatapatikana kwenye tovuti yetu.