Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wakimbizi wa Syria nchini Lebanon kufikia milioni moja na nusu

Idadi ya wakimbizi wa Syria nchini Lebanon kufikia milioni moja na nusu

Idadi ya wakimbizi wa Syria wanaowasili nchini Lebanon inaendelea kuongezeka kila uchao na nchi hiyo huenda ikahifadhi wakimbizi milioni 1.5 mwisho wa mwaka huu.

Kwa mujibu wa mratibu mkaazi wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa nchiniLebanonRossMountainwakimbizi waSyrianchini humo sasa ni asilimia 25 ya idadi ya raia waLebanonhali inayochochea shinikizo la huduma za kijamii na jamii inayohifadhi wakimbizi hao.

Akiongea na waandishi wa habari mjiniGenevaBwanaMountainamesema kuongezeka kwa uwepo wa wakimbizi nchiniSyriakunaongeza vuguvugu hatua inayoweza kusababisha mvutano siku zijazo.

Ameongeza kuwaLebanonhaikuwa tayari kusaidia wakimbizi hao bila ya msaada mkubwa toka jumuiya ya kimataifa.

 “Sehemu kubwa ya wakimbizi wanamiminika sehemu ambazo wanaishi watu maskini Lebanon katika majimbo ya Bekaa na Akkar. Kuna maeneo 225 yanayojumuisha asilimai 86 ya wakimbizi na aslimia 68 ya Walebanon maskini. Matatizo waliyokuwa nayo yameongezeka kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi. Tayari tunaona mvutano kati ya pande hizo mbili. Lakin hofu ambayo wengi wetu tunayo ni kwamba mvutano na sababu nyinginezo kunaweza kuchangaikukuwa kwa mvutano baina ya jamii Lebanon.’’

Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR hadi sasa limesajili wakimbizi waSyriazaidi ya laki tisa nchiniLebanon.