Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uturuki yafungua milango kwa wakimbizi wa Syria kujiunga na vyuo vikuu.

Uturuki yafungua milango kwa wakimbizi wa Syria kujiunga na vyuo vikuu.

Uturuki imeanzisha programu ambamo kwayo wakimbizi wa Syria nchini humo wanaweza kujiunga na vyuo vikuu vya umma bila malipo yoyote ya ada.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema chini ya mpango huo wakimbizi wanaokidhi vigezo wataanza masomo yao kwenye vyuo vikuu saba mwezi Machi mwaka huu.

UNHCR inasema hadi sasa wakimbizi kutoka kambi yaAdiyaman Kusini mwa Uturuki wamejisajili kwa ajili ya maombi ya masomo ambapo 70 ni kwa ajili ya shahada ya kwanza na 10 ni kwa ajili ya shahada ya uzamili.

Kwa sasa Uturuki inahifadhi zaidi ya wakimbizi wa Syria Laki Moja na Elfu Arobaini  waliokimbia mgogoro nchini mwao.