Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW58 wamulikwa

Mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW58 wamulikwa

Mkutano wa 58 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, umeanza mapema wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjiniNew York. Ajenda kuu ni kuangalia hali ya wanawake na wasichana iko vipi wakati huu ambapo malengo ya maendeleo ya milenia yanafikia ukomo mwakani na nini kifanyike kuhakikisha ajenda baada ya mwaka 2015 inazingatia maslahiyaokwa manufaa ya jamii na dunia nzima. Basi ni mambo gani yanafanyika? Ajenda ni zipi zinaibuliwa na kujadiliwa? Hali za makundi maalumi ziko vipi? Ungana basi na Assumpta Massoi kwenye makala hii..