Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wadau wakiwemo wabunge waweka mazingira rafiki kwa wasichana kuhudhuria masomo shuleni mwezi mzima: Tanzania

Wadau wakiwemo wabunge waweka mazingira rafiki kwa wasichana kuhudhuria masomo shuleni mwezi mzima: Tanzania

Mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani unaendelea mjini New York na kando kunafanyika vikao mbali mbali kutathmini mwelekeo wa kundi hilo katika nyanja za kijamii, kisiasa, na kiuchumi. Miongoni mwa vikao hivyo ni kile kilichoangalia nafasi ya wanawake na wasichana katika kuchukua masomo ya sayansi, uhandisi na hesabu. Kikao hicho kilichoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wanawake, UN-Women kilikutanisha wageni na ujumbe kutoka Tanzania ulioelezea hali halisi na hatua zinazochukuliwa kuhamasisha wasichana. Mada ya Tanzania iliwasilishwa na Katibu Mkuu wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Anna Maembe. Katika mahojiano nami Assumpta Massoi nilimuuliza wasilisho lake lilihusu nini?