Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wazidi kuathiriwa na mgogoro nchini Syria: UNICEF

Watoto wazidi kuathiriwa na mgogoro nchini Syria: UNICEF

Mgogoro wa miaka mitatu nchini Syriaumeendelea kusababisha madhila kwa watoto nchini humo, imesema ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Ripoyi hiyo iliyopewa jina "waliozingirwa,  madhara makubwa kwa watoto walioko katika mgogoro kwa miaka miatatuSyria" inasema mgogoro huo umesababaisha athari kubwa kwa watoto milioni 5.5

Ripoti hiyo kadhalika inasema kuwa takribani watoto milioni moja wamekwama katika maeneo ambayo hawawezi kufikishiwa misaada ya kiutu kutokana na kuendelea kwa mzozo na hivyo kuathirika pakubwa.