Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili wa kingono Mashariki ya Kati ukomeshwe: Bangura

Ukatili wa kingono Mashariki ya Kati ukomeshwe: Bangura

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingoni katika maeneo ya vita Zeainab Bangura, amelihutubia baraza la usalama kuhusu ziara yake Mashariki ya Kati ambapo pia wajumbe wa baraza wameelezea masikitiko yao kutokana na kuendelea kwa vitendo  vya utumwa wa ngono na unyanyasaji wa kijinsia katika ukanda  huo.

Wajumbe katika kikao hicho,  wamesema vitendo mathalani ndoa za kulazimishwa kutumika kama mbinu za kivita nchini Iraq, na Syria lazima vikomeshwe na kutaka pande kinzani kulinda raia dhidi ya ukatili wa kingono.

Wamesema kuwa ubakaji na aina  nyingine za ukatili wa kingono katika maeneo ya vita ni uhalifu na vinavunja mkataba wa Geneva. Wametaka jumuiya ya kimataifa kusalia pamoja katika kuwawajibisha wanaohusihwa na uhalifu kama huo.

Kadhalika wajumbe waabaraza la usalama wamesisitiza umuhimu wa pande zote katika ukanda huo wakati wanakabiliana na ugaidi , ujenzi wa amani na kutatua migogoro wazingatie umuhimu wa uwezeshaji wa wanawake na ulinzi dhidi ya wanawake na wasichana wanaokabiliwa na ukatili wa kingono

.

Hata hivyo baraza la usalama wametambua juhudi za nchi jirani katika kulinda wakimbizi ikiwamo dhidi ya ukatili wa kingono na kutaka jumuiya kimataifa kuchangia UM katika kusaidia Syria na Iraq