Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko yaliyozuka upya Syria yatatiza shughili za misaada

Machafuko yaliyozuka upya Syria yatatiza shughili za misaada

Kumejitokeza upya mkwamo wa usambazaji wa huduma za usamaria mwema nchini Syria kufuatia kujitokeza kwa ghasia ambazo zinatatiza shughuli mbalimbali.

Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la utoaji misaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, amesema kuwa mapigano yaliyozuka wiki iliyopita katika maeneo ya Yarmouk yamesababisha hali ya ustawi wa kibinadamu kuzorota.

Msemaji huyo Christopher Gunness amesema kuwa kutokana na hali hiyo,  Umoja wa Mataifa na wahisani wake imenziasha kampeni ikitaka kukomeshwa kwa machafuko hayo ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kusafirishwa.