Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sikio lina mfumo wake wa asili wa kujisafisha, usitumie kitu kingine: Wataalamu

Sikio lina mfumo wake wa asili wa kujisafisha, usitumie kitu kingine: Wataalamu

Wakati dunia leo ikiadhimisha siku ya usafi wa masikio wataalamu wa afya wamesema  kitendo cha mtu kuchokonoa sikio kwa ajili ya kulisafisha ni kinyume na utaratibu ambao mwili wa binadamu umejiwekea ili kusafisha kiungo hicho cha mwili. Watalamu hao akiwemo Dokta Bruno Minja wamesema kitendo cha kuchokonoa kwa kutumia kalamu, pamba, kijiti au kuweka mafuta ya wanyama chaweza kuleta madhara makubwa kwa afya.

(Sauti ya Dokta Bruno)