UNHCR yakaribisha uamuzi wa Burundi kuhusu wakimbizi wa Rwanda

28 Februari 2014

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Burundi limekaribisha uamuzi wa serikali ya nchi hiyo wa kurekebisha hadhi ya ukazi ya raia 37 wa Rwanda waliokimbia nchi yao kati ya Februari 1959 hadi Disemba 1998.

Mwakilishi wa UNHCR Burundi Catherine Huck amesema kundi hilo linahusisha wakimbizi ambao hadhi yao ilisitishwa tarehe 26 February 2014 kufuatia makubaliano ya Geneva ya mwaka 2011 kuhusu wakimbizi wa Rwanda.

Hatua hiyo ya serikali ya Burundi inahusisha mjumuiko wa raia hao kwenye jamii na wengine wameanza mchakato wa kupata vibali vya ukazi bila kusahau kuomba uraia. Hata hivyo kwa wale ambao wanataka kurejea nyumbani kwa hiari nalo pia linafanyika.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter