Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sintofahamu yakumba raia wa Uganda juu ya Muswada kuhusu mapenzi ya jinsia moja

Sintofahamu yakumba raia wa Uganda juu ya Muswada kuhusu mapenzi ya jinsia moja

Nchini Uganda wananchi wamekuwa na maoni tofauti kuhusu sheria inayopinga mapenzi ya jinsia moja baada ya baadhi ya nchi za magharibi kuendelea kutishia kuondoa misaada pale sheria hiyo itakapotiwa saini na Rais Yoweri Museveni. Sheria hiyo pamoja na mambo mengine inawapatia kifungo cha maisha jela wapezi wa jinsia moja. Awali alikataa sheria hiyo akisema adhabu ya maisha jela ni kali mno. Tarifa zaidi na John Kibego wa redio washirika ya Spice FM, nchini Uganda.

(Ripoti ya John Kibego)

Kwenye mkutano wa chama tawala cha NRM wiki iliyopita, Rais Yoweri Museveni aliahidi kutia saini muswada huo wa mwaka 2009. Alisema, alikuwa ameeleweshwa kwamba adhabu kali inaweza tokomeza mapenzi ya jinsia moja ambayo hayaendani na mila na desturi za Kiafrika.

Alikuwa tayari ameonywa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binaadamu asitie sahihi muswada huo. Sasa Barack Obama, raisi wa Marekani ambayo ni mtoaji mkubwa wa misaada kwa Uganda ameonya kuwa uhusiano kati ya nchi yake na Uganda utavurugika ikiwa Museveni atatia saini muswada huo. Wananchi wengi ambao wamekuwa wakipinga kabisa mapenzi hayo sasa wameanza kupingana kwa chaguo. Sheria ipite misaada ikatike? Ama mapenzi yaendelee misaada imiminike?

 (Sauti : John Man, Steven Sabit and Tom Musiime)