Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apongeza hatua iliyopigwa Jamhuri ya Kati

Ban apongeza hatua iliyopigwa Jamhuri ya Kati

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepongeza hatua ya kutangazwa kwa serikali mpya katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR akisema kuwa kuna matumaini ya kupatikana kwa muafaka wa kisiasa.

Ban ameipongeza serikali hiyo ya mpito inayoongozwa na Rais Catherine Samba Panza akisaidiwa na Waziri Mkuu André Nzapayeké ambao tayari wametangaza kusitishwa mapigano na kurejea mezani kwa majadiliano.

Pamoja na kukaribisha hatua hiyo, Ban amerejelea wito wake akisema kuwa Umoja wa Mataifa kamwe haitakaa kando badala yake itaendelea kushirikiana ili kupatikana kwa suluhu ya kudumu.

Hata hivyo ameelezea wasiwasi wake kutokana na mapigano yanayoendelea ambayo yamesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha huku wengine wakilazimika kwenda uhamishoni.