Ban ataka uwekezaji uelekezwe kwa wasichana katika nchi zinazoendelea:

23 Januari 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon hivi sasa dunia inakimbizana na wakati zikiwa zimesalia zaidi ya siku 700 kabla ya ukomo wa malengo ya maendeleo ya milenia hapo 2015. Flora Nducha na maelezo zaidi

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Ban ameyasema hayo Alhamisi kwenye chakula cha mchana kuchagiza mafanikio ya malengo ya maendeleo ya milenia. Ban amesema ni lazima kuchukua hatua kutoa msukumo wa mwisho ili kuhakikisha mafanikio ya amlengo hayo.

Amesema ni lazima kuwekeza kuwapa uwezo wasichana kwa ajili ya kuongeza kasi ya kufikia malengo nah ii inamaanisha ni kuwekeza kwa wasichana zaidi ya nusu bilioni katika nchi zinazoendelea ambao wanaweza kusaidia kusukuma mchakato wa ajenda za malengo ya milenia.

Amesema endapo wasichana watapewa elimu bora, huduma za afya na maisha bora mafanikio yatakuwa zaidi ya mtu mmoja

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Msichana anathamani kubwa katika dunia yetu kama ulivyo mti kwenye msitu. Wakati mti unapokuwa na kuwa imara, mazingira yote yanafaidika. Wakati msichana anakuwa na kuwa shupavu familia yake, jamii yake na hata nchi yake inayahisi mafanikio yake”