UNHCR na serikali ya Uganda wafungua upya kambi kwa ajili ya wakimbizi

21 Januari 2014

Nchini Uganda, kambi ya wakimbizi ya Nyumanzi na ile ya Paratuku zilizo kaskazini mwa nchi hiyo zimefunguliwa upya ili kupatia makazi raia wa Sudan Kusini wanaokimbia vita nchini mwao. Kwa sasa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na serikali ya Uganda wanashirikia kuimarisha kambi hizo kwani tangu mwezi uliopita idadi ya wakimbizi wanaoingia imefikia 50,000. Tarifa zaidi, na John Kbego wa redio wahsirika ya Spice FM, Uganda.

(Tarifa ya John Kibego)

Kambi hizo zilihifadhi maelfu ya Wasudani katika miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoisha mwezi Januari mwaka 2005. Miaka sita baadaye waliokuwa waasi wakajinyakulia uhuru kutoka Sudan na kunda taifa la Sudan Kusini ambalo linakumbwa na vita wenyewe kwa wenyewe.

Kando ya Nyumanzi na Paratuku, Ofisi ya Waziri Mkuu na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), wameunda kambi ya muda ya Nyumanzi.

Kambi ya Dzaipi ambayo ime imekuwa ikitumiwa imeonekana kuzidiwa uwezo wa kuwahifadhi.

Bila shaka, kuna changamoto za kujenga upya vyanzo vya maji, mabarabara na shule miongoni mwa vingine katika makambi yaliokuwa yameondokwa.

Lucy Beck ni Msemaji wa UNHCR nchini Uganda.

(Sauti ya Lucy Beck)

“Siku ya Ijumma tutaanza kuwasafirisha hadi kambi ya pili ya Paratuku. Ni muda mrefu sana kambi hizo hazitumiwi na kwa hiyo tuna changamoto za kujenga shule, vituo vya afia, mabarabara, maji,,.”

Baadhi ya wakimbizi tayari ni wenyeji katika kambi ya Nyumanzi.