Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la kwanza la walinda amani wa kuimarisha UNMISS lawasili Juba

Kundi la kwanza la walinda amani wa kuimarisha UNMISS lawasili Juba

Kundi la kwanza la askari wa kulinda amani wanaopelekwa kuimarisha kikosi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS limewasili kwenye mji mkuuJuba. Kundihilola askari 25 wa Nepal akiwemo afisa mmoja linatoka kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Haiti, MINUSTAH.

Taarifa ya UNMISS inasema kundihiloni tangulizi na litafuatiwa na askari wengine wa Nepal 350 kutoka huko huko Haiti na wanatarajiwa mwishoni mwa mwezi huu. Askari wengine 500 watatoka moja kwa moja Nepal kwenda Sudan Kusini ili kuungana na kundi hilo.

Kamanda Mkuu wa UNMISS Meja Jenerali Johnson Delali Sakyi ametaka askari hao kufanya kaziyaokwa ueledi na kujituma.

Kupelekwa kwa askari hao kunafuatia azimio la baraza la usalama la tarehe 24 Disemba mwaka jana la kuongoza askari 5,500 ili UNMISS iwe na jumla ya askari 12,500.

Kwa mujibu wa UNMISS mashauriano yanaendelea ili kupata askari wengine kutoka Ghana, Rwanda, India, Bangladesh na Tanzania.