Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yasambaza zaidi ya tani 125 za vifaa vya tiba Aleppo

WHO yasambaza zaidi ya tani 125 za vifaa vya tiba Aleppo

Shirika la afya duniani, WHO limesema katika kipindi cha wiki mbili zilizopita limesambaza zaidi ya tani 125 ya vifaa tiba hukoAlepponchiniSyriaikiwa ni kwenye maeneo yanayodhibitiwa na serikali na pia vikundi vya upinzani. Taarifa ya WHO imesema vifaa hivyo ni pamoja na vile vya upasuaji, dawa za kutibu magonjwa ya kuambukiza, vifaa vya kusaidia watoto njiti na vitanda kwa ajili ya wodi za wagonjwa mahututi.

Shehena ya kwanza ilikuwa ni kwa ajili ya wagonjwa 55,000 kwenye hospitali ya mafunzo ya tibaAleppoilhali ile ya pili iliwasilishwa kwa mashirika ya kiraia, mamlaka za afya eneohilopamoja na shirika la hilali nyekundu yaSyriakwa ajili ya wagonjwa Laki Mbili na Elfu Kumi na Tatu.

Hali ya usalama nchiniSyriaimekuwa ikizorota tangu kuanza kwa mzozo huo miaka mitatu iliyopita na kusababisha uhaba wa vifaa tiba na hata wahudumu wa afya huku hospitali na zahanati zikishambuliwa na kuharibiwa. WHO imetaka pande zote husika kwenye mzozo waSyriakuheshimu sheria za kimataifa ikiwemo mkataba waGeneva, unaotaka ulinzi kwa watumishi wa afya, wagonjwa na vituo vya afya.