Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wahaha CAR, wajihifadhi hekaluni!

Wakimbizi wahaha CAR, wajihifadhi hekaluni!

Wakati ripoti zinasema hali bado si shwari katika mzozo unaoendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, inaelezwa kuwa maelfu kwa maelfu ya raia wanaendelea kupoteza makazi wakikimbia machafuko nchini humo.

Baadhi ya raia wa nchi hiyo sasa wanakimbilia katika nyumba za ibada ili kujihifadhi. Chakula na afya ni changamoto kubwa kwa jamii hizi huku wanawake na watoto wakiteseka zaidi. Ungana na Joseph Msami katika ripoti ifuatayo.