Hatimaye Fao yawapatia mbegu wakulima huko Ufilipino

17 Disemba 2013

Mwezi mmoja baada ya kimbunga Haiyan kupiga nchini Ufilipino, shirika la kilimo na chakula duniani, FAO limewapatia mbegu wakulima wa kisiwa cha Visayan ambao walipoteza mazaoyaona vifaa vingine muhimu baada ya janga hilo.

Tayari usambazaji wa mbegu hizo muhimu umeanza ambapo FAO na idara ya kilimo Ufilipino wanawapatia wakulima mbegu kwa ajili ya kilimo cha mpunga na mahindi.

Mwakilishi mkazi wa FAO nchini humo Rodriguez Vinet amesema wanafurahi kuwa wameweza kurejesha matumaini kwa wakulima kwa ajili ya msimu huu wa upanzi na hata kuwa na uhakika wa mavuno  mwezi Machi na Aprili.

Amesema wakulima walipoteza jamaa namalizao lakini angalau uhakika wa mbegu kwa ajili ya kilimo unaweza kuwahakikishia kurejesha maishayaona kujipatia kipato

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter