Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio huko Aleppo laitia hofu UNICEF

Shambulio huko Aleppo laitia hofu UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasema lina wasiwasi mkubwa juu ya ripoti kuwa shambulio la anga lililofanyika Jumapili huko Aleppo penginepo limesababisha vifo vya watoto kati ya 14 na 28.

Mkurugenzi wa Shirika hilo kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Maria Calvis amesema katika taarifa yake akizingitia ripoti ya kwamba mabomu yaliangushwa kutoka kwenye helikopta jijiniAleppo.

Amesema ni kitendo kisichokubalika kwa watoto kuwa walengwa kwa njia ya shambulio la jumla au kwa njia yoyote ile. Bi. Calvis amesema UNICEF inarejelea wito wake wa kutaka pande zote kuzingatia sheria za kimataifa za kulinda raia ikiwemo watoto kwenye maeneo ya mizozo.