Siku ya haki za binadamu, OPCW yakadhibiwa tuzo ya Nobel, ILO yalilia haki za wafanyakazi

10 Disemba 2013

Katika kuadhimisha siku ya haki za binadamu duniani hii leo, mashirika mbali mbali ya Umoja wa Mataifa yameangazia ukiukwaji wa haki za binadamu katika sekta mbali mbali ikiwemo ile ya afya, ajira huku siku hii hii ya leo ikimulikwa wakati shirika la kimataifa la kupinga silaha za kemikali, OPCW,  ikipokea tuzo yake huko Oslo Norway. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

(Ripoti ya Grace)

Mjini OSLO,Norway, miaka 20 iliyopita.. Nelson Mandela na F.W de Klerk, kwa muongozo wa wimbo huu waliingia katika ukumbi kupokea tuzo ya amani  ya Nobel, kwa kusimamia haki, kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu na hatimaye kuweka misingi ya amani nchini mwao, na leo ilikuwa ni Ahmet Üzümcü mkuu wa OPCW na Kamati ya tuzo hiyo wakiingia tayari kumkabidhi tuzo hiyo….

OPCW imeongoza jitihada za ukaguzi wa silaha za kemikali nchiniSyriana baada ya kupokea tuzo hiyo Bwana Uzumcu akazungumza…

(Sauti ya Ahmet)

“Ninatoa shukrani kwa wale wote ambao kupitia kujitolea kwao na kwa uamuzi ambao wamechangia katika mafanikio haya ya kutokomeza silaha za kemikali na ninapongeza serikali kwa  mtizamo wao na kwa kuchukua hatua hii imara.”

 Katika hatua nyingine shirika la kazi duniani, ILO limetaka kutokomezwa kwa ukiuwakji wa haki za wafanyakazi duniani ambao Milioni 400 ni maskini wa kupindukia. Nayo Global Fund imetaka vikwazo vyote vya kufikia haki ya tiba viondolewe.