Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na waziri wa mambo ya nje wa Panama:

Ban akutana na waziri wa mambo ya nje wa Panama:

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Panama bwana Fernando Núñez Fábrega.

Katika mazungumzo yao wamejadili maendeleo ya kiuchumi ya Panama, athari za upanuzi wa mrfereji wa Panama na masuala mengine ya kiusalama yahusuyo ajenda za Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu ameishukuru serikali ya Panama kwa mchango wake katika kituo cha Umoja wa mataifa cha kikanda na cha kiufundi kinachohusika na misaada ya kibinadamu ambacho sasa kinajengwa.