Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni Wakati wa kutoa mchango wa kweli kukabiliana na tabia nchi: Mtaalam wa UM

Ni Wakati wa kutoa mchango wa kweli kukabiliana na tabia nchi: Mtaalam wa UM

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu na mshikamamo wa pamoja duniani Virginia Dandan, amezitaka nchi kutoa michango ya kweli ili kukabiliana na tatizo la tabia nchi.

 George Njogopa na taarifa kamili

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

Wito wa Bi Dandan umekuja katika wakati ambapo wataalamu wa majadiliano ya mapatano kutoka mataifa zaidi ya 190 wakikutana huko Warsaw katika kile kinachoelezwa kuwa ni jaribio la kutupa karata muhimu kuwezesha mataifa kufikia makubaliano ya pamoja ya kukabiliana na kishindo cha mabaidliko ya tabia nchi.

Akizungumzia umuhimu wa wapatanishi hap, mtaalamu huyo aliwakumbusha wajibu waliona akisema kuwa wanapaswa kuweka misingi itayosaka majawabu kuhusu hali ya dunia na siyo kujikita katika eneo moja pekee.

Kwa upande mwingine aligusia mkutano wa mawaziri wanaotazamia kukutana kuanzia Novemba 20 huko huko Warsaw kujadilia upatikanaji wa vyanzo vya fedha kwa ajili ya kufadhilia miradi inayohusu agenda ya mabadiliko ya tabia nchi.

Alisema mawaziri hao wanalojukumu la kubainisha bayana vyanzo vya mapato kwa ajili ya kusukuma mbele agenda ya mabadiliko ya tabia nchi katika siku za usoni.