Afrika yatakiwa kuimarisha mifumo ya kuwalinda watoto:UNICEF

6 Novemba 2013

Mashirika kumi na tatu yakiwamo ya  Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi barani Afrika yametoa wito kwa serikali barani humo kuimarisha mifumo ya ulinzi kwa watoto ili kuwalinda dhidi ya ukatili, unyanyasaji, kutelekezwa na unyonyaji katika mazingira ya dharura na yasiyo ya dharura.

 (TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Taarifa ya mashirika hayo ikiwamo lile la kuhudumia watoto , UNICEF pamoja na mtandao wa asasi imesema utekezwaji wa haki ya ulinzi kwa watoto utachangia katika kukuza  maendeleo ya kiuchumi na agenda ya kupunguza umaskini barani Afrika.

Akizungumza kwa niaba ya mashirika hayo mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la sera ya mtoto wa Afika, ACPF Théophane Nikyèma, ameongeza kuwa watoto wakilindwa wanaweza kukwepa matatizo ya kiafya kadhalika.

Mashirika  yanatarajiwa kutoa mapendeklezoyaokatika amkutano mjini Adis Ababa Ethipoia utakaoangazia haki na ustawi wa watoto ambapo kauli mbiu katika mkutano huo ni: ikiwa watoto wanalindwa dhidi ya  ukatili, unyanyasaji, kutelekezwa na unyonyaji wanaweza kuhudhuria shule na kuongeza uwezo wao katika masomo.