Uhalifu wa kimazingira unaathiri usalama na maendeleo:UNEP/INTERPOL

6 Novemba 2013

Uhalifu dhidi ya mazingira unaoanzia biashara haramu ya bidhaa za wanyamapori na mbao , biashara haramu ya bidhaa zinazoharibu tabaka la ozoni na uvuvi ulio haramu ni changamoto la kimataifa ambalo athari zake ni kubwa. Haya yote yamejadiliwa  kwenye mkutano uliondaliwa mjini Nairobi Kenya kati ya shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na polisi wa kimataifa INTERPOL. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

 (RIPOTI YA JASON)

Uhalifu kwa mazingira huathiri sekta nyingi na mara nyingi uhusishwa na ukiukaji wa haki za binadamu, ghasia, mizozo, ulanguzi wa pesa, ufisadi na mitandao ya uhalifu ya kimataifa kwa mujibu wa utafiti kutoka kwa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na polisi wa kimataifa INTERPOL.

Uhalifu dhidi ya wanyamapori pekee unakadiriwa kugharimu kati ya dola bilioni 15 na 20 kila mwaka na unaorodheshwa kuwa wa nne nyuma ya biashara ya madawa ya kulevya ya binadamu na silaha.

Utafiti unaonyesha kuwa biashara haramu ya wanyamapori na mbao inaweza kufadhili vitendo vya kigaidi na uhalifu mwingine kote duniani. Achim Steiner na mkurugenzi mkuu wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP.

 (SAUTI YA ACHIM STEINER)