Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sigrid Kaag awa mratibu maalum wa ujumbe wa pamoja kuhusu Syria

Sigrid Kaag awa mratibu maalum wa ujumbe wa pamoja kuhusu Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la kupinga matumizi ya silaha za kemikali duniani, OPCW wamemteua Bi. Sigrid Kaag  kutoka Uholanzi kuwa mratibu maalum wa ujumbe wa pamoja wa pande mbili hizo linalosimamia uteketezajiwa silaha za kemikali Syria.

Akizungumza na waandishi wa habari mjiniNew York, siku ya Jumatano wakati akimtambulisha Bi. Kaag, Bwana Ban amemwelezea kuwa na uzoefu mkubwa na ameshukuru kuwa tayari Baraza la Usalama limeidhinisha jinalakenahivyo kuonyesha umuhimu wa suala la Syria. Bwana Ban ametaja majukumu ya Mratibu huyo maalum….

“Majukumu yake ni pamoja na kuhakikisha usalama wa wakaguzi wa OPCW pamoja na upatikanaji wa vifaa vyao,, mawasiliano, afya na hata masuala ya usaidizi kwenye maeneo ambapo Umoja wa Mataifa una uwezo wa kufanya hivyo. Halikadhalika Bi. Kaag ataratibu usaidizi wa kimataifa kusaidia kutokomeza mpango wa silaha za kemikali wa Syria kwa mujibu wa maamuzi ya Baraza la Usalama na baraza tendaji la OPCW.”

Katibu Mkuu amesema changamoto zinafahamika, hali nchini Syria bado ni ya hatari na  haitabiriki na kwamba ushirikiano wa pande zote nchini humo ni muhimu.  Katika mkutano huo Bi. Kaaga alipata fursa ya kuzungumza na kuelezea shukrani zake.

(Sauti ya Bi. Kaag)

Mratibu huyo maalum ana shahada ya uzamili ya falsafa ya mahusiano ya kimataifa na anazungumza kiingereza, kifaransa, kijerumani na kiarabu.