Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nyerere ni dira ya dunia: Watanzania

Nyerere ni dira ya dunia: Watanzania

Baadhi ya wananchi waTanzania waliohudhuria hafla ya kwanza ya kumbukumbu ya miaka 14 tangu kifo cha mwasisi wa taifa hilo marehemu Julius Nyerere wamesema kiongozi huyo ataendelea kubakia lama ya umoja,maendeleo na hata ukombozi wa elimu Afrika na duniani.

 Wakiongea katika mahojiano na Joseph Msami wa idhaa hii wananchi hao wamesema kiongozi huyo alitamka mambo ambayo sasa ni dira ya dunia katika maendeleo mathalani malengo ya milenia ya sasa na baada ya mwaka 2015.

 (Sauti Mahojiano)