Kunahitajika uwekezaji zaidi wa kifedha kukabili changamoto za mabadiliko ya tabia nchi-Ban

14 Oktoba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitolea mwito Jumuiya ya Kimataifa kuwekeza zaidi katika teknolojia ya vyombo vya fedha ili kukabiliana na tabia ya mabadiliko ya tabia nchi akisema kuwa wakati unakimbia kukabilia changamoto zizotokana na mabaidiko hayo.

Akisisitiza zaidi, Ban amezitaka jumuiya hizo kuowanisha mifumo ya kisera pamoja na mienendo ya ufanyaji kazi kwani bila kufanya hivyo itakuwa vigumu kukamilisha malengo ya dunia.

Amesema kuwa suala la mabadiliko ya tabia nchi ni kitisho kinachoziandama nchi zite duniani hiyo zinawajibu w akusaka suluhu ya pamoja. Amesema suala la maendeleo endelevu likabiliwa na changamoto kubwa hivyo kutatuliwa kwa changamoto hiyo kunahitaji mashirikiano ya pamoja.

Ameongeza kusema kuwa kadri changamoto za kiuchumi zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi zinavyoendelea kukua ndivyo inavyohitajika kuchukuliwa tahadhari zaidi.