Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano mapya DRC, Baraza la usalama latoa kauli

Mapigano mapya DRC, Baraza la usalama latoa kauli

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wameshutumu kuzuka upya kwa mashambulio huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongo, DRC yaliyosababisha kifo cha mlinda amani kutokaTanzaniana majeruhi. Taarifa ya barazahiloiliyotolewa Alhamisi baada ya kupokea ripoti kutoka kwa Naibu Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu operesheni za ulinzi wa amani, Edmond Mulet imetaka serikali ya DRC kuchunguza tukiohilona wahusika wafikishwe mbele ya sheria. Limetaka vikundi vya waasi vikiwemo M23 na FDLR kuacha mara moja mashambulio na ghasia ya aina yoyote la sivyo halitasita kuweka vikwazo zaidi dhidi ya wanaokiuka vikwazo vya awali.  Kuhusu makombora yanayodaiwa kurushwa kutoka DRC kwendaRwanda, Baraza limeonyesha wasiwasi na kutaka mfumo wa pamoja wa kufuatilia hali ya mpakani kuchunguza madai hayo. Baraza limesisitiza kuwa harakati zozote za kukwamisha mamlaka ya MONUSCO hazitavumiliwa na kwa mantiki hiyo limeunga mkono agizo la Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko  DRC Martin Kobler Kobler la kutaka kikosi cha MONUSCO kuchukua hatua zozote kulinda raia.