Ban awataka viongozi kuchukua hatua zaidi kufikia malengo ya kutokomeza umasikini:

21 Agosti 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka viongozi wa dunia kuchukua hatua madhubuti ya kufikia malengo ya kutokomeza umasikini na mchakato endelevu. Ban ametoa ripoti muhimu kabla ya mkutano wa viongozi wa dunia utakaofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York tarehe 25 Septemba. Ripoti hiyo inatanabaisha nini kinachohitajika kufanyika kuchapuza juhudi za kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ifikapo 2015 na pia kuelezea ajebnda mpya ya dunia ya maendeleo baada ya 2015.

Ripoti hiyo mpya inaitwa “Maisha ya hadhi kwa wote” na mtu aliefanya kazi kwa karibu na Ban kufanikisha ripoti hiyo ni mshauri maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu mipango ya maendeleo ya baada ya 2015 ni Bi Amina Mohammed ambaye ameeleza vipengee muhimu vya ripoti hiyo

(CLIP YA AMINA MOHAMMED)