Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa umezindua mradi wa kimataifa kukabiliana na njaa

Umoja wa Mataifa umezindua mradi wa kimataifa kukabiliana na njaa

Shirika la chakula na kilomo duniani FAO linazindua mradi wa kupambana na tatizo la njaa duniani kwa ajili ya maslahi ya wote.

Mradi huo ni kampeni ya kimataifa na utatumia mtandao na kuwachagiza watu kutokaa kimya kuhusu tatizo la njaa ambalo linaatghiri watu wengi duniani hususani kutoka nchi zinazoendelea. Kauli mbiu ya mradi huo ni "njaa kwa watu bilioni moja" na wanatumaini utatoa fursa kwa watu kuelezea jinsi wanavyokasirishwa na kusikitishwa kuwa katika karne hii ya 21 zaidi ya watu bilioni moja hawana chakula cha kutosha.

Kwa kufanya hivyo FAO inaamini kuwa hatua mbalimbali zitachukuliwa ili kukabiliana na tatizo hilo kabla halijatoa athari kubwa zaidi.