Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azungumzia wito wa SADC juu ya vikwazo dhidi ya Zimbabwe

Ban azungumzia wito wa SADC juu ya vikwazo dhidi ya Zimbabwe

Hatma yoyote kuhusu vikwazo dhidi ya Zimbabwe ni kitu ambacho kinapaswa kujadiliwa na nchi wanachama au vyombo vya kikanda husika, ni kauli ya Katibu Mkuu Ban Ki-Moon aliyotoa leo mjiniNew York, Marekani wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu ziara zake alizofanya Mashariki ya Kati na huko Pakistani. Kauli hiyo inafuatia swali la mwandishi wa habari aliyetaka kufahamu msimamo wa Bwana Ban kuhusu tamko la jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC la kutaka kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Rais Robert Mugabe na baadhi ya viongozi pamoja na matokeo ya uchaguzi wa hivi karibuni nchini humo.  Katibu Mkuu amesema kuhusu uchaguzi amezingatia matokeo na kwamba amekuwa akisihi serikali na Rais Mugabe kuhakikisha uchaguzi ni huru na haki.

 (SAUTI YA BAN)

 “Ni matumaini  yangu kwamba utata wote ule au tathmini za sasa kutoka makundi mbali mbali vitaakisi kwa kina utashi wa wananchi kwa mujibu wa misingi ya kimataifa ya demokrasia.”

 Wakati huo huo imeelezwa kwamba Katibu Mkuu anaanza Jumatano ataanza ziara Korea Kusini ambapo Ijumaa atakuwa na mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo akiwemoRaisParkGeun-hye.