Wataalamu wa UM wawasili Nairobi kubaini athari za moto kwenye uwanja wa ndege

14 Agosti 2013

 

Jopo la wataalamu kutoka Umoja wa Mataifa limewasili nchini Kenya kufuatia ombi la serikali ya nchi hiyo kwa ajili ya kuchunguza athari za mazingira zinazoweza kuwa zimesababishwa na moto uliokumba eneo la wageni wanaowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wiki iliyopita. Jason Nyakundi na taarifa kamili

TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)

Wataalamu hao wataendesha utafiti kuhusu athari za kimazingira zilizosababishwa na moto huo. Wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa pia watatoa usaidizi kwa serikali katika oparesheni za kusafisha eneo lililoteketea kuhakikisha kuwa hakuna madhara yoyote kwa mazingira.

Pia wanatarajiwa kutambua hatua za kiusalama zinazohotaji kuchukuliwa wakati ya kubuniwa kwa vituo vya muda vya kutoa huduma na njia za kukabiliana na athari za kimazingira zinazotokana na moto huo. Kundi hilo la wataalamu lilibuniwa kupitia ushirikiano wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa  OCHA iliyo na makao yake mjini Geneva. Ripoti kamili ya matokeo ya uchunguzi huo itachapishwa mwishoni mwa shughuli hiyo.