Ofisi ya masomo ya utafsiri yafunguliwa Nairobi

26 Julai 2013

Ufunguzi rasmi wa ofisi inayojulikana kama InZone yenye madhumuni ya kufundisha tafsiri ya lugha mbali mbali barani Afrika umefanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi,Kenya.Mafunzo haya yanalenga wale wanaohudumu katika nchi ambazo zimekumbwa na vita, na athari zinazoletwa na hali hiyo. Kufunguliwa kwa ofisi hiyo kunasisitiza umuhimu unaopewa na Umoja wa Mataifa juu ya lugha na matumizi yake katika kukuza amani , usalama na maendeleo.

Ufunguzi huo unafuatia uamuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Nairobi (UNON) mwaka jana  Bi Sahel-Work Zewde wa kufungua kituo cha Kutafsiri cha nchi za Afrika (PAMCIT) kwenye ofisi hizo. Rajab Luhangela David kutoka DRC ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo.

(SAUTI YA Rajab)

Lugha ambazo Bwana Rajabu anatafsiri  ni Kiswahili , Kibembe, Lingala na Kifaransa.