Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA na EU washirikiana katika elimu kwenye dharura:

UNRWA na EU washirikiana katika elimu kwenye dharura:

Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limekuwa likifanya kazi kutoa msaada wa elimu na kisaikolojia kwa watoto wa wakimbizi wengi wa Kipalestina ambao wametawanywa na machafuko Syria.

Sasa UNRWA inapigwa jeki na Muungano wa Ulaya katika suala hili. George Njogopa na taarifa kamili

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

Msaada kutoka Jumuiya ya Ulaya ambayo hadi sasa imechangia kiasi cha euro milioni 2.4, imeliwezesha shirika hilo kuandaa na kutekeleza miradi inayolenga kukwamua sekta ya elimu kupitia kile kinachoitwa utoaji elimu ya kisaikolojia ili kuwasaidia watoto ambao wapo katika makundi hatarishi kutokana na vita

UNRWRA imekuwa ikiendesha programu zake katika maeneo yote ambayo kunakutikana wanafunzi waliolazimika kwenda mtawanyikoni kutokana na kuzuka kwa mapigano ya mara kwa mara.

Pia UNWRA imefanikiza zoezi la utambuzi katika nchi za Syria, Lebanon na Jordan na kuanzisha vituo maalumu kwa ajili ya kukusanya watoto waliokosa makwao na kisha kuwahimiza kurejea shuleni.

Mwezi Aprili mwaka huu shirika hilo liliendesha mafunzo ya siku tano huko Amman ambayo yalikuwa na shabaha ya kuwajengea uwezo washiriki.