Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi saba barani Afrika zapunguza maambukizi ya Ukimwi kwa watoto: UNAIDS

Nchi saba barani Afrika zapunguza maambukizi ya Ukimwi kwa watoto: UNAIDS

Ripoti mpya kuhusu mipango ya kimataifa ya kupunguza na kumaliza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi miongoni mwa watoto ifikapo mwaka 2015 na kuwaongozea maisha mama zao imeonyesha hatua zilizopigwa katika kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi miongoni mwa watoto barani Afrika . Assumpta massoi anaripoti.

 (RIPOTI YA ASSUMPTA MASSOI)

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa nchi saba zilizo kusini mwa jangwa la Sahara zikiwemo Botswana , Ethiopia, Ghana, Malawi  na Afrika Kusini zimepunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi miongoni mwa watoto kwa asilimia 50 tangu mwaka 2009 huku mataifa mengine mawili Tanzania na zambia nayo yakipiga hatua. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa kulikuwa na visa 130,000 vya maambukizi ya virusi vya ukimwi miongoni mwa watoto kwenye nchi hizo vikipungua kwa asilimia 38 tangu mwaka 2009. Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kupambana na ukinjwa wa ukimwi la Umoja wa Mataifa UNAIDS Michel Sidibe anasema kuwa hatua zilizopigwa kwenye nchi nyingi ni ishara tosha kuwa iwapo masuala muhimu yatazingatiwa watoto wanaweza kuzaliwa bila ya virusi vya ukimwi.