Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yayatambua rasmi mataifa 38 yaliyopunguza njaa kwa asilimia 50:

FAO yayatambua rasmi mataifa 38 yaliyopunguza njaa kwa asilimia 50:

Mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO José Graziano da Silva ameyatambua rasmi mataifa 38 yaliyofannikiwa kupungua njaa kwa nusu wakati tukielekea ukomo wa malengo ya maendeleo ya milenia hapo 2015.

Katika hafla maalumu iliyoghudhuriwa na wakuu wa nchi mbalimbali,nchi18 zimepokea diploma ya mafanikio ya mapema ya kufikia lengo la kkwanza la milenia la kupunguza kwa nusu njaa ifikapo mwaka 2015 na lengo la mkutano wa kimataifa wa chakula la kupunguza kwa nusu idadi ya watu wnaokabiliwa na njaa ifikapo 2015.

Nchi hizo ni Armenia, Azerbaijan, Cuba, Djibouti, Georgia, Ghana, Guyana, Kuwait, Kyrgyzstan, Nicaragua, Peru, Saint Vincent na Grenada, Samoa, Sao Tome na Principe, Thailand, Turkmenistan, Venezuela na Viet Nam.

Nchi nyingine 20 zoimepokea diploma ya kufikia lengo la kwanza tuu ambazo ni Algeria, Angola, Bangladesh, Benin, Brazil, Cambodia, Cameroon, Chile, Dominican Republic, Fiji, Honduras, Indonesia, Jordan, Malawi, Maldives, Niger, Nigeria, Panama, Togo na Uruguay.