Msaada wa UNHCR wafika Al Raqqa nchini Syria

14 Juni 2013

Huduma za Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR zimefika Al Raqqa  eneo lililo kaskazini mwaSyriaambalo imekuwa vigumu kulifikia kwa muda wa miezi mitatu iliyopita na ambapo hali ya kibinadamu inaripotiwa kuwa mbaya. Alice Kariuki anaripoti

(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)

Msaada huo utawasaidia karibu watu 5000 waliohama makwao eneohilo. Pia makundi ya UNHCR nchiniLebanonyanaendelea na shuhuli za kuandiskisha na kuwasaidia wakimbizi wanaowasili kutoka mji unaokumbwa na ghasia wa  Al-Qusayr nchiniSyria. Melissa Flemming ni msemji wa UNHCR.

(SAUTI YA MELISSA FLEMMING)

Familia zilizozungumza na UNHCR zinautaja mji wa Al-Qusayr kuwa ulioharibiwa na kubaki mahame. Mmoja wao  alisema kuwa hwkuna chakula kilichosalia kwenye mji huo na hata maji haipatikani.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter