Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yashukuru Japan kupanua wigo wa shughuli za ulinzi wa amani Sudan Kusini

UNMISS yashukuru Japan kupanua wigo wa shughuli za ulinzi wa amani Sudan Kusini

Tunapenda kushukuru serikali ya Japan kwa kupanua wigo wa shughuli zake za ulinzi wa amani nchini Sudan Kusini, hiyo ni kauli ya Hilde Johnson Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa ofisi ya Umoja huo nchini Sudan Kusini, UNMISS aliyotoa kufuatia uamuzi wa Japan wa kupanua eneo la shughuli zake nchini humo. Katika taarifa yake Bi. Johnson amesema  wakati huu ambapo dunia inakaribia kuadhimisha siku ya walinda amani, wanapongeza uamuzi wa Japan wa kuongeza maeneo ya shughuli zake na kwamba barabara na huduma za usafirishaji ni muhimu katika ujenzi wa amani Sudan Kusini. Kwa sasa kampuni ya Uhandisi ya Japan ikiwa na askari 330 iko mji mkuu Juba na viunga vyake na maandalizi yanaendelea ili mwezi ujao iweze kupeleka askari hao kwenye majimbo ya Equitoria Mashariki na Magharibi. Japan ilichukua uamuzi huo baada ya mashauriano yaliyofanyika mjiniNew Yorkbaina yake na UNMISS na sekretarieti ya Umoja wa Mataifa.