Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasaidia kurejea makwao wavuvi wa Kenya waliokwama Puntland

IOM yasaidia kurejea makwao wavuvi wa Kenya waliokwama Puntland

Mabaharia sita raia wa Kenya waliokuwa wametelekezwa na mwajiri wao kwenye eneo la Basaso Puntland nchini Somalia mwezi Novemba mwaka 2012 watarejea nyumbani  kesho Jumatano kupitia msaada wa Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Wavuvi hao ambao walikuwa kati ya kundi lililokuwa ndani mwa chombo kimoja cha uvuvi waliondoka mjini Mombasa Kenya kwa shughuli ya uvuvi ya siku kumi  kwenye bahari ya Hindi ambapo baadaye walitia nanga kwenye bandari ya Kismayo. 

Meli yao  kisha ikaelekekea mjini Mogadishu ambapo nahodha wake alitoweka na kuwaacha wavuvi pamoja na meli bila sababu yoyote. Kisha meli hiyo ilipata rubani mwingine lakini ikakikumbwa na hitilafu za kimitambo na kutia nanga kwenye bandari ya Bosaso.  

Ililazimu wizara inayohusika na masuala ya usafiri wa bahari eneo la Puntland kuingilia kati na kuliomba shirika la IOM kuchukua hatua kuwasaidia wavuvi hao kurudi nyumbani.