Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Angola, Namibia na Afrika Kusini zatiliana saini matumizi endelevu ya mkondo wa Benguela

Angola, Namibia na Afrika Kusini zatiliana saini matumizi endelevu ya mkondo wa Benguela

Angola, Namibia na Afrika Kusini zimekubaliana kushirikiana ili kutumia vyema mkondo wa Benguela ambao una moja ya mifumo ya ekolojia yenye rasilimali nyingi zaidi duniani kwa manufaa ya nchi hiyo na wakazi wanaoutegemea kwa maisha yao.

Mkondo huo ulioko bahari ya Atlaniki, una rasilimali nyingi za baharini pamoja na kutumika kwa huduma kama vile usafirishaji na bidhaa zitokanazo nao zinakadiriwa kuwa thamani ya zaidi ya dola Bilioni 54 kwa mwaka.

Kwa mantiki hiyo nchi hizo tatu katika makubaliano yao zimeahidi kulinda na kuhifadhi mazingira ya mkondo huo na eneo linalozunguka ambao shughuli zake ni pamoja na uchimbaji wa mafuta na gesi, usafirishaji, utalii wa pwani na uvuvi wa kibiashara.

Mkuu wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP nchini Angola, Maria do Valle Ribeiro amesema makubaliano hayo ni njia bora zaidi na fanisi ya kufanikisha matumizi endelevu ya mkondo huo kwa vizazi vya sasa na hata vizazi vijavyo vinavyoutegemea.