Hammarskjöld akumbukwa alivyojitolea kulinda amani

10 Aprili 2013

Umoja wa Mataifa leo umekuwa na kumbukumbu maalum ya miaka 60 tangu kula kiapo kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa umoja huo Dag Hammarskjöld aliyefariki dunia katika ajali ya ndege mwaka 1961 wakati akielekeaCongokwenye masuala ya amani. Shughuli hiyo imehudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Katibu Mkuu wa sasa Ban Ki-Moon ambaye katika hotuba yake amesema Hammarskjöld  anakumbukwa vile alivyojitolea uhai wake kwa ajili ya kulinda amani. Amesema kumbukumbu hii imekuja wakati ambapo walinda amani wa Umoja wa Mataifa wameuawa huko Sudan Kusini na kwamba siku ya leo inakumbusha hatari inayowakabili wale waliojitoa uhai wao kulinda wengine.

 (

(SAUTI YA BAN)

 “Wahusika wa vitendo hivyo ni lazima wawaadhibiwe kwa uhalifu wao. Na katika kumbukumbu ya leo inatukumbusha hatari inayowakabili wale wanaotumikia Umoja wa Mataifa. Tangu kifo cha  Dag Hammarskjöld, maelfu ya wafanyakazi na walinda amani wamepoteza maisha yao wakati wakihudumu kwa niaba ya Umoja wa Mataifa. Hata hivyo mchango wao unaendelea kutambuliwa kutokana na kazi inayoendelezwa na wenzao kwa minajili ya amani.” 

Washiriki wa kumbukumbu hiyo walisikiliza hotuba aliyotoa Hammarskjöld wakati wa kuapishwa kwake miaka 60 iliyopita.

 (SAUTI YA Hammarskjöld )

“Lakini nimejaribu kudokeza hisia  ambazo kwazo nitazitumia kufanya kazi yangu pindi nitakapotakiwa kushiriki kwenye  jitihada zozote za  Umoja wa Mataifa za kufanikisha matumaini ya  wanachama wake.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter