Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhifadhi wa misitu ni suala nyeti katika maendeleo ya kiuchumi

Uhifadhi wa misitu ni suala nyeti katika maendeleo ya kiuchumi

Mkutano wa kimataifa kuhusu mustakhbali wa misitu duniani umeanza hii leo huko Istanbul Uturuki ambapo ajenda kuu ni jinsi gani uhifadhi wa misitu unaweza kusaidia kuchochea maendeleo ya kiuchumi.

Theluthi moja ya eneo la dunia ni misitu na takribani watu bilioni Moja na Nusu wanategemea misitu kwa maisha yao ya kila siku.

Msaidizi wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya uchumi na kijamii Wu Hongbo amesema hii ni fursa ya kipekee ya kutambua jinsi ya kuendeleza rasilimali hiyo ya kipekee duniani.

(SAUTI YA HONGBO)